Tunafungua Milango ya Fursa

Tunarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha, maarifa na teknolojia ili kusaidia watu, biashara na jamii kukua.

Woman holding her baby while standing with other community members in Tanzania
Tulivyoanza

Yote Yalianza na Mama Mmoja

Impact Microfinance ilianza kutokana na maisha ya mama mjane mwenye watoto watatu, aliyefanya kazi kwa bidii kuwahudumia watoto wake, lakini bado alihangaika kukidhi mahitaji yao ya msingi.

Juhudi na uvumilivu wake vilitufanya tujiulize swali rahisi: Nini kingebadilika ikiwa watu wangepata mtaji, maarifa na uhuru wa kuamua wenyewe mahitaji yao muhimu zaidi?

Tulianza na wanawake 40, kila mmoja akipata dola 100 za Marekani pamoja na elimu ya fedha, bila kuwapangia jinsi ya kutumia fedha hizo. Tulifuatilia safari zao ili kuelewa maamuzi waliyofanya.

Ndani ya miezi mitatu, asilimia 90 walikuwa wameanzisha shughuli za kuwaingizia kipato. Wengine walitumia msaada huo kukidhi mahitaji muhimu kama matibabu na kuboresha makazi yao.

Uzoefu huo ndio msingi wa Impact Microfinance ya leo. Tunaendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha, maarifa na teknolojia ili watu wengi zaidi wawezekuwa na maisha bora.

Ni imani yetu kuwa watu wanapopata fursa na nyenzo sahihi, wanaweza kuboresha maisha yao na kujenga kesho bora zaidi.

Tufahamu

Tunawezesha Jamii. Tunajenga Kesho Bora.

Tunasogeza huduma za kifedha, maarifa na teknolojia karibu nawe ili uweze kufikia fursa mpya, kukuza biashara yako na kuboresha maisha yako.

Kwa kushirikiana na jamii na wadau wa maendeleo, tunawawezesha wajasiriamali, wakulima na familia kuongeza kipato, kutengeneza ajira na kufungua fursa kwa wengine.

Two Maasai women wearing colourful traditional clothing during a community gathering in Tanzania

Uwezeshaji

Tunawapa watu nyenzo na kujiamini ili waweze kusimamia mustakabali wao wa kifedha.

Ujumuishi

Tunabuni suluhisho za kifedha zinazowafikia watu na jamii ambazo hazijafikiwa vya kutosha na huduma za kifedha.

Ubunifu

Tunatumia teknolojia na mawazo bunifu kurahisisha huduma za kifedha na kuzifanya zipatikane kwa urahisi zaidi.

Uadilifu

Tunazingatia uwazi, uwajibikaji na uadilifu katika kila jambo tunalofanya.

Ushirikiano

Tunashirikiana na jamii na washirika wetu ili kuleta matokeo bora na ya kudumu.

Uendelevu

Tunabuni suluhisho zinazojenga uimara wa kiuchumi wa muda mrefu na kuchochea ukuaji wenye uwajibikaji.
Portrait of Gershom Mpangalah, Founder and CEO of Impact Microfinance

Gershom Mpangalah

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu
Portrait of Issa Ngwegwe, Co-Founder and Executive Director of Impact Microfinance

Issa Ngwegwe

Mwazilishi na Mkurugenzi
Portrait of Halifa Mjengwa, Technology Advisor at Impact Microfinance

Halifa Mjengwa

Mshauri wa Teknoojia
Portrait of Tom Kocsis, Director and Expansion Advisor at Impact Microfinance

Tom Kocsis

Mkurugenzi wa Bodi
Portrait of Maclean Michael Kamala, Director and Compliance Advisor at Impact Microfinance

Maclean Kamala

Mkurugenzi wa Bodi
Dhamira Yetu

Kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha, maarifa na teknolojia ili watu na jamii ziweze kustawi.

Two Maasai women wearing colourful traditional clothing during a community gathering in Tanzania
Dira Yetu

Kujenga mustakabali wenye ushirikishwaji wa kifedha, ambapo hakuna anayeachwa nyuma.

Maadili Yetu

Uwezeshaji

Tunatoa nyenzo na msaada unaohitajika ili kuwawezesha watu kusimamia fedha zao na kujenga mustakabali bora wa kifedha.

Ujumuishi

Tumejizatiti kuwafikia watu na jamii ambazo hazijafikiwa vya kutosha na huduma za kifedha, ili kuhakikisha kila mmoja anapata fursa za kifedha.

Ubunifu

Tunatumia teknolojia na suluhisho bunifu kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongeza ufanisi wake.

Uendelevu

Tunalenga kuleta matokeo chanya ya muda mrefu katika uchumi na mazingira kupitia shughuli na mipango yetu yote.

Uadilifu

Tunazingatia uwazi, uaminifu na uwajibikaji katika mahusiano na shughuli zetu zote.

Ushirikiano

Tunaamini katika nguvu ya ushirikiano na suluhisho zinazotokana na jamii ili kuleta matokeo chanya na ya kudumu
Timu Yetu
Nguvu Iliyo Nyuma ya Impact Microfinance.
Portrait of Gershom Mpangalah, Founder and CEO of Impact Microfinance

Gershom Mpangalah

Mwanzilishi Mwenza na Mkurugenzi Mkuu
Portrait of Issa Ngwegwe, Co-Founder and Executive Director of Impact Microfinance

Issa Ngwegwe

Mwanzilishi na Mkrugenzi
Portrait of Halifa Mjengwa, Technology Advisor at Impact Microfinance

Halifa Mjengwa

Mshauri wa Tekinolojia
Portrait of Tom Kocsis, Director and Expansion Advisor at Impact Microfinance

Tom Kocsis

Mkuugenzi wa Bodi na Mshauri Ukuaji
Portrait of Maclean Michael Kamala, Director and Compliance Advisor at Impact Microfinance

Maclean Kamala

Mkurugenzi wa Bodi
Huduma Zetu

Fedha. Maarifa. Teknolojia.

Kupitia huduma za kifedha, teknolojia, elimu ya fedha na ujasiriamali, tunawawezesha wafanyabiashara, wakulima na jamii kwa ujumla kufikia malengo yao na kuboresha maisha.

Huduma zetu zimeundwa kulingana na mahitaji halisi, kuanzia upatikanaji wa mitaji, uwezo wa kusimamia fedha zako hadi njia za kidijitali za kusimamia vikundi vya akiba na mikopo.

Mikopo

Pata mikopo ya kukuza biashara, kuwekeza kwenye kilimo, kuimarisha mtiririko wa fedha au kukidhi mahitaji muhimu.
Angalia Mikopo

Elimu

Pata maarifa, ujuzi na uwezo wa kusimamia fedha zako, kukuza biashara na kufanya maamuzi bora ya kifedha.
Angalia Mafunzo

Pamoja

Rahisisha usimamizi wa vikundi vya akiba na mikopo kupitia mfumo wa kidijitali unaowezesha wanachama kuweka akiba, kupata mikopo na kusimamia shughuli za vikundi kwa uwazi na ufanisi.
Fahamu Pamoja
Washirika

Tushirikiane Kupanua Huduma za Kifedha. Tuongeze Matokeo Chanya.

Shirikiana nasi kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha, hususani vijijini, kutoa elimu ya fedha na kufikisha teknolojia kwa jamii ambazo hazijafikiwa ipasavyo.

Kwa pamoja, tunaweza kufikisha huduma zenye matokeo chanya kwa jamii nyingi zaidi na kutengeneza fursa endelevu za kiuchumi.

Shirikiana Nasi
Mitaji Inayokuza Biashara.
‍Ushirikiano Wenye Tija kwa Wengi.
Ajira

Jenga Taaluma Yako. Leta Mabadiliko.

Shiriki kutengeneza bidhaa na kutoa huduma zinazopanua upatikanaji wa huduma za kifedha kwa jamii ambazo hazijafikiwa vya kutosha.

Jiunge na timu yetu inayosukumwa na dhamira ya dhati, ubunifu na matokeo chanya yanayopimika.

Utamaduni Wetu

Tunaamini mawazo bora hukua kupitia ushirikiano, uwajibikaji na kuheshimiana. Tunawapa wafanyakazi wetu fursa ya kuchangia mawazo, kukuza uwezo wao na kuleta mabadiliko chanya.

Uwezeshaji
Ushirikishwaji
Ubunifu
Uko Tayari Kuleta Mabadiliko?
Jiunge Nasi

Njia za Kuleta Mabadiliko

Shirikiana nasi kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha, kuimarisha jamii na kuleta fursa endelevu za kiuchumi.

Shirikiana Nasi

Shirikiana na Impact Microfinance kufikisha huduma za kifedha, teknolojia na programu za maendeleo kwa jamii ambazo hazijafikiwa vya kutosha.
Fahamu Ushirikiano

Wekeza Katika Mabadiliko

Toa mtaji unaosaidia kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha, kukuza biashara na kujenga fursa endelevu za kiuchumi.
Fursa za Uwekezaji

Tushirikishe Wazo Lako

Una programu, jamii, soko au fursa ambayo Impact Microfinance inaweza kuchangia maendeleo? Tushirikiane kuona tunachoweza kujenga pamoja.
Wasiliana Nasi

Tuwasiliane

Have Una swell, maoni, fursa ya ushirikiano au wazo? Tutafurahi kusikia kutuka kwako.

Lazima
Lazima
Silazima
Asante! Tumepokea ujumbe wako. Tutawasiliana nawe hivi karibuni.
Samahani, ujumbe wako haukutumwa. Tafadhali jaribu tena au wasiliana nasi kupitia info@impactmicrofinance.com