Pamoja ni mfumo wa kidijitali unaosaidia vikundi na taasisi za wanachama kusimamia shughuli, kukusanya rasilimali, kutunza kumbukumbu, kuimarisha uongozi shirikishi na kupata huduma za kifedha kupitia jukwaa moja.
Omba demoIngia Pamoja
Pamoja ni mfumo wa kidijitali unaosaidia vikundi na taasisi za wanachama kusimamia shughuli, wanachama, rasilimali, kumbukumbu za michango na huduma za kifedha, huku ukiimarisha uongozi shirikishi.
Wanachama wanaweza kutumia Pamoja kupitia App, USSD na Web. Mfumo huu hurahisisha shughuli za kila siku, huongeza uwazi, ufanisi kusaidia jamii kukua kwa uendelevu.

Pamoja inalenga kurahisisha usimamizi wa vikundi na taasisi za wanachama, kuongeza uwazi, kuimarisha uongozi na ushiriki wa wanachama, na kusaidia jamii kukua kwa uendelevu kupitia teknolojia..
Unaoimarisha uongozi, ujumuishaji katika huduma za kifedha na ukuaji endelevu.
Kurahisisha shughuli, kuimarisha ushiriki wa wanachama na kusaidia ukuaji endelevu..
Jamii ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Pamoja inaimarisha mifumo ambayo jamii tayari inaitumia, kwa kuboresha uwazi na ufanisi wa uongozi, usimamizi wa wanachama na tarifa zao, ukusanyaji wa rasilimali, na upatikanaji wa huduma za kifedha.
Jamii ndiyo kitovu cha shughuli na maamuzi yote.
Ndani ya Pamoja jamii inaendelea kumiliki, kuongoza na kusimamia shughuli zake.
Teknolojia inayoimarisha mifumo ya jamii badala ya kuibadilisha.
Kuimarisha uwazi, uwajibikaji na uaminifu ndani ya jamii.
Vikundi via kijamii na taasisi nyingine za wanachama tayari zimeunganisha wanachama pamoja, zinakusanya michango na Akiba za wanachama wake na kusaidiana kila siku. Kadiri vinavyozidi kukua, matumizi ya kumbukumbu za karatasi, fedha taslimu na mifumo ya kazi za mikono hufanyao usimamizi kwa mgumu, hupunguza uwazi na kuongeza hatari na hasara zisizo za lazima.
Kadiri idadi ya wanachama, miamala na shughuli zinavyoongezeka, kumbukumbu za Kwenye karatasi huwa ngumu kutunza na kuongeza wezekano wa makosa na kutoelewana.
Mtumizi ya fedha taslimu huongeza hatari ya upotevu wa fedha, hupunguza uwazi na kufanya uhakiki wa miamala kura mgumu zaidi.
Maombi, idhini na mikutano inayosimamiwa kwa njia za kawaida inaweza kuchelewesha shughuli. Ukosefu wa taarifa za kutosha pia hufanya maamuzi na uwajibikaji kuwa mgumu zaidi.
Jamii hujenga uaminifu kupitia michango, uongozi na marejesho ya mikopo. Hata hivyo, bila kumbukumbu za kidijitali zinazoaminika, uwezo wenu wa kifedha unaweza kushindwa kutambulika.
Pamoja inaunganisha mifumo ambayo jamii tayari inaitumia katika jukwaa moja la kidijitali. Inadumisha uaminifu uliopo huku ikiongeza uwazi, ufanisi na upatikanaji wa huduma za kifedha.
Jamii nyingi hutegemea kumbukumbu za karatasi, fedha taslimu na taratibu za kawaida ambazo huwa ngumu kusimamia kadiri shughuli zinavyoongezeka.
Jamii zinasimamia shughuli zao kupitia jukwaa moja salama na lililounganishwa kidijitali.
Pamoja inaunganisha huduma muhimu kwa jamii katika jukwaa moja la kidijitali. Inarahisisha usimamizi wa wanachama, ukusanyaji wa rasilimali, miamala, upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongeza uwazi katika shughuli za kila siku.
Simamia wanachama, taarifa zao, majukumu na kumbukumbu katika hatua zote za uanachama.
Simamia michango, akiba, hisa na rasilimali nyingine za wanachama kwa urahisi.
Simamia makusanyo, marejesho na malipo kupitia mifumo iliyounganishwa..
Imarisha uongozi, uidinishaji na utoaji wa taarifa kwa maamuzi bora.
Jamii imara hujenga uchumi imara. Pamoja inasaidia vikundi na taasisi za wanachama kuongeza uwazi, ushiriki na uwajibikaji, huku ikipanua upatikanaji wa huduma za kifedha na teknolojia zinazochochea ukuaji endelevu.
Kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za kifedha na fursa kwa jamii mbalimbali husa zile za kipato cha chini, bila kujali mahali zilipo.
Kuimarisha uaminifu kupitia kumbukumbu salama, uongozi bora na taarifa za wakati halisi.
Kuwawezesha wanachama kushiriki, kufanya maamuzi bora na kujenga jamii imara na endelevu.
Pamoja inaunganisha wanachama, michango, miamala, uongozi bora na kumbukumbu katika jukwaa moja la kidijitali. Inaongeza uwazi, upatikanaji wa taarifa kwa wakati halisi na uwezo wa jamii kuendesha shughuli na kukua kwa uhakika pasipo migogoro itokanayo na upotevu wa kumbukumbu.
Kupunguza hatari za matumizi ya fedha taslimu, kuongeza uwazi na kuimarisha uaminifu kupitia taarifa sahihi na kwa wakati.
Kuimarisha uongozi, kuongeza uwazi na ufanisi, upatikanaji wa huduma kwa wakati na kusaidia ukuaji endelevu.
Kuongeza ushiriki, uwazi, upatikanaji wa huduma za kifedha na ushirikiano wa wanachama.
Kuunganisha wanachama, kuongeza ushiriki, kusogeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kuimarisha matawi.
Kuongeza uwazi wa shughuli, kuimarisha uwajibikaji na kufuatilia matokeo kwa washirika wao.
Kuunganisha wanachama, kuimarisha uongozi na kuratibu ukuaji.
Pamoja inamwezesha kila mwanachama kushiriki kupitia simu janja, kompyuta au simu ya kawaida. Hii inarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wote, popote jamii zilipo.
Huduma kamili za kidijitali kwa wanachama na viongozi wa jamii.
Tumia Pamoja kupitia simu yoyote ya mkononi, hata bila intaneti.
Simamia shughuli za jamii na taarifa zake kupitia mfumo mmoja.
Pata mwongozo na msaada unapouhitaji katika kutumia Pamoja.
Pamoja inaunganisha vikundi vya kijamii, taasisi za wanachama na washirika, mifumo ya malipo, huduma za kifedha na teknolojia za kidijitali kupitia jukwaa moja, na hivyo kufungua fursa zaidi kwa vikundi, wanachama na jamii kwa ujumla.
Pamoja inasaidia jamii katika kila hatua kwa kuunganisha shughuli zao, kukusanya rasilimali, kuimarisha uongozi na kuweka msingi wa ukuaji endelevu.
Unganisha wanachama na shughuli zao katika mfumo mmoja.
Kusanya na simamia rasilimali za wanachama kwa ufanisi na uwazi.
Imarisha uwajibikaji na ushiriki wa wanachama.
Jenga uimara na fursa za maendeleo ya kudumu.
Pata majibu, jifunze jinsi ya kuanza kutumia Pamoja na upate msaada unaohitaji ili kunufaika kikamilifu na huduma zetu.
Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu Pamoja.
Pamoja ni mfumo wa kidijitali kwa vikundi vya kijamii na taasisi za wanachama. Unasaidia kusimamia wanachama, akiba, hisa, mikopo, mikutano, uongozi na taarifa kupitia jukwaa moja salama.
Pamoja imeundwa kwa vikundi vya kijamii, vyama vya ushirika, vikundi vya akiba, taasisi za kidini, klabu za michezo, mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi nyingine za wanachama.
Wanachama wanaweza kujiunga kupitia programu ya simu, USSD au mfumo wa wavuti, kwa mwaliko kutoka kwa kiongozi wa kikundi kulingana na utaratibu wa taasisi husika.
Kila kikundi hupewa namba maalumu ya utambulisho, na kila mwanachama aliyeidhinishwa hupata namba yake ya kipekee. Huduma zinapatikana kwa wanachama waliothibitishwa na kuidhinishwa kwa kufuata taratibu za kikundi.
Ndiyo. Pamoja inapatikana pia kupitia USSD, hivyo wanachama wenye simu za kawaida wanaweza kutumia huduma muhimu bila intaneti.
Ndiyo. Pamoja hutumia mifumo salama ya uthibitishaji, udhibiti wa ruhusa kulingana na majukumu na teknolojia ya usimbaji fiche ili kusaidia kulinda taarifa za kikundi.
Unaweza kusimamia wanachama, akiba, hisa, mikopo, mikutano, uongozi, ushiriki, taarifa na bidhaa za kikundi kupitia mfumo mmoja.
Mwanachama anaweza kuwasilisha ombi la kujitoa kupitia mfumo. Ombi hufuata taratibu za kikundi za uongozi na uidhinishaji, huku akiba, hisa, mikopo na wajibu mwingine vikishughulikiwa kwa mujibu wa kanuni za kikundi.
Unaweza kuwasiliana na timu yetu kupitia tovuti, barua pepe au WhatsApp. Tutakusaidia kuanza na kujibu maswali yako.
Ndiyo. Vikundi na taasisi vinaweza kuweka bidhaa, taratibu za kazi, kanuni za uongozi na ruhusa za watumiaji kulingana na mahitaji yao.
Timu yetu ipo tayari kukusaidia kuanza, kusajili wanachama na kujibu maswali yako kabla na baada ya kuanza kutumia Pamoja.
Fahamu jinsi Pamoja inavyoweza kusaidia kikundi au jamii yako kurahisisha shughuli, kuimarisha uongozi na kukusanya rasilimali.